ODM YASHINIKIZA HAKI KWA WAATHIRIWA
Tukiwa bado katika masuala ya haki, chama cha ODM kimeitaka serikali kuharakisha fidia kwa familia zilizowapoteza wapendwa wao wakati wa maandamano nchini jinsi ilivyokubalika katika mkataba wa maelewano ya kisiasa baina ya chama hicho na UDA.
Wito huo ulitolewa kwenye hafla ya kumkumbuka aliyekuwa kinara wa ODM Raila Odinga, viongozi wakiitaka mahakama kuweka mbele haki kwa waathiriwa katika kesi ya kupinga kubuniwa kwa jopokazi la kushughulikia fidia hiyo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































