#Local News

KAULI YA SHOLLEI

Naibu spika wa bunge la kitaifa Gladys Shollei amehoji kuwa uchaguzi ndogo unaotarajiwa kufanyika maeneo mbalimbali ni mtihiani muhimu kwa makamishina wapya wa  tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC walioteuliwa hivi karibuni.

Akizungumza na kituo kimoja cha runinga nchini Shollei amependekeza kuwa chaguzi hizo zinawapa maafisa hao wa IEBC fursa ya kuimarisha utendekazi na kutambua maeneo ya kuboreshwa kabla ya uchaguzi mkuu wa 2027.

Aidha amewapongeza makamishina hao kwa hatua ambayo walichukua kuwatoza faini wagombeaji wa eneo bunge la Kasipul baada  ya vurugu kati ya wafuasi wao na kusababisha vifo vya watu watatu.

Imetayarishwa na Shadrack Maina

KAULI YA SHOLLEI

NYARIBO ATIMULIWA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *