VURUGU ZAWAACHA MAKUMI NA MAJERAHA KISII
Makumi ya watu wanaendelea kuuguza majeraha kufuatia makabiliano baina ya makundi mawili ya vijana katika maeneo ya Keroka na Kisii muda mfupi kabla ya viongozi wa upinzani kuandaa mikutano ya hadhara maeneo hayo hapo jana.
Mikutano hiyo ilikuwa imeandaliwa na naibu kinara wa Jubilee Fred Matinag’i, ambaye amewalaumu polisi na wanasiasa wanaoegemea chama tawala cha UDA eneo hilo kwa madai ya kufadhili vurugu hizo ili kuvuruga mikutano hiyo.
Hata hivyo, wameapa kuungana kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 














































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































