MZEE AHUKUMIWA MAISHA KWA KUMNAJISI MJUKUU WAKE BUNGOMA
Mzee Mmoja kwa jina la Benson Kitui amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumnajisi mjukuu wake mwenye umri wa miaka kumi Tukio linaloripotiwa kutokea katika eneo la Sasur, kaunti ndogo ya Cheptais, kaunti ya Bungoma.
Kitui alifikishwa mbele ya Mahakama ya Sirisia, ambapo hukumu hiyo ilisomwa, ikionyesha msimamo mkali wa mahakama dhidi ya vitendo vya unyanyasaji wa kingono, hasa vinapofanywa ndani ya familia.
Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Sirisia, Raymond Lang’at, amesema upande wa mashtaka uliweza kuthibitisha kesi hiyo bila kuacha shaka yoyote, na kwamba kosa hilo lilistahili adhabu ya juu zaidi chini ya sheria za Kenya.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































