MWONGOZO WA SHA KUSITISHA ‘UTALII WA KIMATIBABU’
Ni huduma za matibabu ambazo hazipatikani nchini pekee ndizo zitagharamiwa na mamlaka ya afya ya jamii SHA nje ya nchi, katika mwongozo mpya ambao umetolewa na mamlaka hiyo katika juhudi za kuziba mianya ya ufisadi na kuhakikisha fedha za umma zinatumika ipasavyo.
Katika mwongozo huo, SHA imetangaza kugharamia upasuaji 36 pekee nje ya nchi kama vile upandikizaji wa ini, figo za Watoto, matibabu ya kisasa ya saratani, upasuaji tata wa moyo na tiba ya seli kwa ufadhili wa hadi shilingi elfu 500.
Waziri wa afya Aden Duale, amesema matibabu ya nje ya nchi yalikuwa yamegeuzwa biashara.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































