UFISADI UNAANGAMIZA NCHI- MARAGA, KIGAME
Serikali imetakiwa kuvunja kimya chake kuhusu kudorora kwa sekta muhimu kama vile afya na elimu ya juu, ambayo imedorora kutokana na mgomo wa wahadhiri wa vyuo vikuu vya umma.
Wakizunguza katika hafla moja kaunti ya Makueni, jaji mkuu wa zamani David Maraga na mwimbaji wa nyimbo za injili Reuben Kigame, wamehusisha changamoto zinazoikabili nchi na ufisadi katika sekta mbali mbali.
Wawili hao waliotangaza azma ya kuwania urais, wamesema watatatua changamoto hizo iwapo watachaguliwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































