SERIKALI, UPINZANI WALAUMIANA MBEERE
Serikali na muungano wa upinzani wameendelea kulaumiana kuhusu vurugu zinazoshuhudiwa kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa Mbeere North, macho sasa yakielekezwa kwa idara ya usalama kuingilia kati huku uchaguzi huo ukikaribia.
Akizungumza kwenye misururu ya kampeni eneo hilo, naibu Rais Kithure Kindiki amemshtumu mtangulizi wake Rigathi Gachagua kwa madai ya kufadhili makundi ya vijana kuvuruga amani, kauli yake ikijiri huku muungano huo ukidai serikali ina njama ya kuvuruga uchaguzi huo.
Kulingana na Kindiki, Gachagua alifeli katika majukumu yake kama naibu rais.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































