#Sports

KIKOSI CHA TAEKWONDO ROHO JUU LICHA MWANZO MBOVU

Timu ya taifa ya mchezo wa Taekwondo imedumisha matumaini ya kufanya vyema licha ya mwanzo mbaya katika mashindano ya dunia ya mchezo huo kwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 yaani World U21 Taekwondo Championships yaliyoanza rasmi hapo jana ugani Kasarani jijini Nairobi.

Pambano hilo la wiki moja limewavutia wachezaji wachanga kutoka pembe zote za dunia, na hivyo kuweka ushindani wa kiwango cha juu kwa mataifa yanayoshiriki.

Kikosi cha Kenya kinachowakilishwa na mataekwondoin 4 ambao ni Willias Odhiambo, Vivian Shali, Festos Mbalala na Waida Mula, kilikabiliwa na ushindani mkali katika raundi zao za kwanza na licha ya kuonyesha mbinu kali na ueledi, wote 4 walilemewa na kubanduliwa mapema baada ya kupoteza pointi kwa wapinzani wao.

Kocha mkuu Samuel Kinyanjui, amepongeza kikosi chake kwa juhudi zao na kujitolea, akikiri changamoto za kushiriki kipute cha kiwango cha dunia.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

KIKOSI CHA TAEKWONDO ROHO JUU LICHA MWANZO MBOVU

NYOTA WA AFRIKA WAONGEZEWA WIKI NA FIFA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *