#Business

OGAMBA AKANA MADAI YA KUTOLEWA KSH1.1B KWA SHULE HEWA

Waziri wa Elimu Julius Ogamba amepuuzilia mbali madai kwamba serikali ilitoa Ksh1.1 bilioni kwa shule hewa.

Kulingana na ripoti ogamba amefafanua kuwa matamshi yake Bungeni yalitafsiriwa vibaya, akieleza kuwa pesa hizo hazijatolewa kwa sababu takriban shule 990 zilikosa kuwasilisha data inayohitajika ili kuthibitishwa.

Kufuatia hali hiyo, Wizara ilitoa asilimia 50 tu ya shule kwa baadhi ya shule. Ogamba aidha amehakikishia umma kuwa data sahihi itatolewa mara tu zoezi la uhakiki litakapokamilika.

Imetayarishwa na Maurine Amwayi

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *