#Local News

UPINZANI WATISHIA MASHTAKA BINAFSI DHIDI YA POLISI 12

Muungano wa upinzani umefutilia mbali mikutano yake na Inspekta mkuu wa Polisi Douglas Kanja, na badala yake utawafungulia mashtaka ya jinai maafisa 12 wa polisi na wabunge wawili kutoka kaunti za Murang’a na Nyeri kuhusiana na uvamizi dhidi ya kanisa moja wakati wa ibada iliyokuwa ikihudhuriwa na aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua katika kaunti ya Nyeri mwezi jana.

Kupitia taarifa iliyotiwa saini na Gachagua, vinara wenza Kalonzo Musyoka, Fred Matiang’i na Eugene Wamalwa, muungano huo umesema hauna imani tena na uongozi wa idara ya polisi, ukidai kuwa tayari uchunguzi dhidi ya uvamizi huo umekamilika, ila faili iliyokuwa iwasilishwe kwa mkurugenzi wa mashtaka ya umma umetekwa na Waziri wa usalama wa kitaifa Kipchumba Murkomen akiagiza kwamba hakuna mashtaka yatakayofunguliwa.

Sasa wameapa kuanzisha mashtaka hayo mara moja, huku wakiwaonya polisi dhidi ya kuvuruga mikutano ya kisiasa iliyopangwa katika kaunti za Kisii, Nyamira, Nakuru na Nairobi.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

UPINZANI WATISHIA MASHTAKA BINAFSI DHIDI YA POLISI 12

CHARLES KANJAMA RAIS MPYA LSK

UPINZANI WATISHIA MASHTAKA BINAFSI DHIDI YA POLISI 12

KAMATI YA ELIMU YATOA AGIZO KWA TSC

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *