#Business

MAONYESHO YA KILIMO YANG’OA NANGA JIJINI NAIROBI

Maonyesho ya Kimataifa ya Kilimo barani Afrika ya mwaka 2025 yamefunguliwa rasmi jijini Nairobi, chini ya kauli mbiu “Kuongeza Uzalishaji wa Kilimo barani Afrika kupitia Uvumbuzi na Upatikanaji wa Soko” kwa lengo la kuboresha ushirikiano wa China na Afrika katika kilimo cha kisasa.

Katibu wa Kilimo nchini Paul Kipronoh Ronoh amesema maonyesho hayo yanalenga kuiweka Afrika kama kituo cha kimataifa cha uvumbuzi wa kilimo na biashara.

Ronoh aidha amesema maonyesho hayo yamekutanisha washiriki zaidi ya 150, wakiwemo 100 kutoka China, na hivyo kuwakilisha hatua kubwa inayoonyesha ukuaji wa nafasi ya Kenya kama kituo cha kikanda cha uvumbuzi wa kilimo na biashara.

Imetayarishwa na Maurine Amwayi

MAONYESHO YA KILIMO YANG’OA NANGA JIJINI NAIROBI

RAUNDI YA 4 YA CARABAO KUMALIZIKA LEO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *