MURKOMEN APONGEZA MAAFISA 230 WA POLISI KUTOKA HAITI
Waziri wa Usalama wa Taifa Kipchumba Murkomen amewapongeza maafisa wa polisi wa Kenya waliokuwa wametumwa nchini Haiti katika jukumu la kudumisha amani.
Murkomen amesema kuwa Kenya, kama mwanachama wa Umoja wa Mataifa, ina jukumu la kushiriki katika operesheni za kurejesha amani katika mataifa yanayokumbwa na ghasia na machafuko.
Maafisa 230 wa polisi waliorejea nchini juzi walikuwa sehemu ya kikosi kilichotumwa Haiti kusaidia katika kurejesha utulivu katikati ya machafuko yanayoendelea nchini humo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































