NAPOLI WASHINDA ITALIAN SUPER CUP
David Neres aliifungia Napoli mara 2 na kuwapa ubingwa wa kombe la Italian Super Cup katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Bologna kwenye fainali jana usiku.
Wing’a huyo wa Brazil aliwaweka Napoli kifua mbele kabla ya kipindi cha kwanza kutamatika baada ya kupinda mpira kutoka mbali, kabla ya kushambulia tena kutokana na makosa ya kipa wa Bologna Federico Ravaglia na kuwapa mabingwa hao wa Serie A ushindi dhidi ya mabingwa watetezi wa Italian Super Cup.
Taji hilo ni la 3 kwa Napoli ambao waliibandua AC Milan kwenye nusu fainali wiki jana.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































