#Football #Sports

GOR WALAZIMISHWA KUTOA SARE

Klabu ya Gor Mahia ilitoka sare ya bao 1:1 na Ulinzi Stars katika mchuano wa ligi kuu KPL kwenye uwanja wa michezo wa Kasarani hapo jana.

Gor walianza vyema mchezo na kutamalaki kwa kipindi kirefu, ushirikiano wa Shariff Musa na Austin Odhiambo ukiwatatiza mabeki wa Ulinzi Stars, kabla ya juhudi zao kuzaa matunda katika dakika ya 6 wakati Felix Oluoch aliwaweka kifua mbele.

Hata hivyo, Ulinzi waliwatia pingu Green Commandos kupitia kwa mchezaji Boniface Muchiri kunako dakika ya 34.

Matokeo hayo yamewaacha Gor katika nafasi ya 2 na kuendeleza msururu wa kutopoteza mechi, nao Ulinzi wakifarijika katika nafasi ya 16.

Katika matokeo mengine, AFC Leopards waliwakwaruza Mathare United kwa kichapo cha mabao 2-0, Murang’a Seal wakiwaadhibu KCB kwa mabao 2-1, huku limbukeni Nairobi United wakikaribishwa nyumbani kwa kichapo cha mabao 3 bila jibu mikononi mwa Sofapaka.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *