#Football #Sports

DROO YA CARABAO CUP- ARSENAL, CITY, CHELSEA, PALACE, NEWCASTLE

Manchester City watachuana na bingwa mtetezi wa Carabao Cup Newcastle United katika nusu fainali za kipute hicho, zitakazochezwa kwa mikondo miwili nyumbani na ugenini mapema mwaka ujao.

City walijikatia tiketi jana usiku kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Brentford, na kutinga nusu fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 2021, ambapo kabla ya hapo, walikuwa wameshinda taji hilo mara 4 mfululizo.

Mabao ya kiungo wa Ufaransa Rayan Cherki na wing’a wa Brazil Savinho yaliwahakikishia ushindi, meneja Pep Guardiola akiwapumzisha wachezaji muhimu kama Erling Haaland, mabeki Josko Gvardiol, Reuben Diaz na kipa Gianluigi Donnarumma.

Nao Newcastle waliingia awamu hiyo baada ya kushinda mabao 2-1 dhidi ya Fulham.

Chelsea ambao walifuzu Jumanne usiku, watasubiri mshindi wa pambano lililoahirishwa kati ya Arsenal na Crystal Palace.

Pambano hilo ambalo litachezwa Jumanne ijayo, liliahirishwa ili kuwaondolea Palace mzigo wa kucheza mechi 3 katika mud awa siku 5, ikizingatiwa kuwa walikuwa na mechi ya UEFA Conference League Alhamisi wiki jana.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

DROO YA CARABAO CUP- ARSENAL, CITY, CHELSEA, PALACE, NEWCASTLE

AKONNOR ASHUSHA PUMZI KUFUATIA USHINDI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *