#Football #Sports

NYOTA WAJAA MWONDOANO AFCON

Wachezaji mahiri wamesheheni raundi ya mwondoano ya timu 16 za mwisho katika kipute cha taifa bingwa barani Afrika AFCON 2025 nchini Morocco, raundi hiyo inapoanza hapo kesho.

Miongoni mwa nyota hao ni beki wa PSG na mchezaji bora wa Afrika mwaka jana Achraf Hakimi anayeiwakilsha Morocco, fowadi wa Liverpool Mohammed Salah anayeisaidia Misri kusaka taji la 8 la AFCON na Mshambulizi wa Galatasaray Victor Osimhen, anayeongoza safu ya mashambulizi ya Nigeria wanaposaka taji hilo baada ya kubanduliwa kwenye fainali na Ivory Coast mwaka 2024.

Mechi hizo za mwondoano zenye mvuto ni Senegal dhidi ya Sudan, Mali dhidi ya Tunisia, Morocco dhidi ya Tanzania, Morocco wakijivunia mashambulizi makali yanayoongozwa na Brahim Diaz ambaye anaongoza kwa ufungaji wa mabao akiwa na 3 sawa na Riyadh Mahrez wa Algeria.

Mechi nyingine ni Afrika Kusini dhidi ya Cameroon, Misri dhidi ya Benin, bingwa mtetezi Ivory Coast dhidi ya Burkina Faso, Algeria dhidi ya DR Congo na Nigeria dhidi ya Msumbuji.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

NYOTA WAJAA MWONDOANO AFCON

CITY WATIWA BREKI EPL

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *