DUALE AKANUSHA KUPOTEA KWA SH BILIONI 50 ZA SHA
Waziri wa Afya Aden Duale amekanusha madai kwamba shilingi bilioni 50 zilipotea katika Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA), akisema takwimu zilizochapishwa katika moja ya magazeti ya humu nchini zilipotoshwa.
Duale amesema taarifa hizo zilitokana na kutoeleweka kwa taratibu za uhasibu wa kisheria pamoja na mchakato wa mpito wa kifedha.
Katika taarifa yake, amesema kiasi kilichoonekana kama malipo ya kutiliwa shaka ni makadirio ya kawaida ya uhasibu, mafao yaliyoidhinishwa kisheria pamoja na uhamisho wa kawaida wa fedha benki wakati wa mpito kutoka NHIF hadi SHA.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































