KEPSHA YAWAKWAMIA WALIMU WA JSS
Muungano wa walimu wakuu wa shule za msingi KEPSHA umepinga pendekezo la walimu wa sekondari msingi JSS kuhamishiwa chini ya usimamizi wa shule za upili, ukiwataka walimu hao kuepusha siasa za miungano ya walimu kwenye uendeshaji wa shule.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa muungano huo Fuad Ali, uamuzi wa JSS kuwa chini ya shule za msingi uliafikiwa kufuatia jopokazi la rais kuhusu elimu na kwamba washikadau wote walishirikishwa.
Ameyasema haya kwenye kongamano linaloendelea jijini Mombasa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































