SERIKALI YASAMBAZA CHAKULA CHA MSAADA TURKANA
Zaidi ya wakazi 300,000 wanaokabiliwa na makali ya njaa kutokana na ukame katika kaunti ya Turkana wanatarajia kupata msaada wa chakula ambacho kimeanza kusambazwa na serikali kuu katika juhudi za kudhibiti makali ya njaa.
Kwa mujibu wa Waziri wa utumishi wa umma Geoffrey Ruku, serikali imetuma malori 21 yenye chakula hicho kikiwemo cha Watoto wachanga, akina mama wanaonyonyesha pamoja na mifugo.
Amesema waathiriwa pia watapewa fedha kupitia mpango wa Inua Jamii.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































