#Local News

UDA, ODM ZADUMISHA VITI

Vyama vya serikali jumuishi ambavyo ni UDA na ODM vimedumisha nyingi ya viti vyake katika chaguzi ndogo za ubunge zilizoandaliwa jana, mgombeaji wa ODM katika eneo bunge la Kasipul Boyd Were akishinda kwa kura 16,819, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Philip Aroko aliyepata kura 8,476.

Katika eneo bunge la Mbeere North, Leo Wamuthende wa UDA ameibuka mshindi kwa kura 15,802 na kumbwaga Newton Karish wa chama cha DP aliyepata kura 15,308.

Kwenye eneo bunge la Magarini, Harison Kombe wa ODM anaongoza katika matokeo yaliyotangazwa, mbele ya Stanley Kenga wa DCP huku Moses Omondi wa ODM akitangazwa mshindi katika eneo bunge la Ugunja.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

UDA, ODM ZADUMISHA VITI

UPA YAONYESHA UDA KIVUMBI NYAMIRA

UDA, ODM ZADUMISHA VITI

WAMUTHENDE: NITAWATUMIKIA WOTE

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *