#Football #Sports

MAN CITY WASHINDA HUKU BARCELONA WAKISHIKWA

Klabu ya Manchester City ilipata ushindi wa mabao 4-1 kiulaini dhidi ya Borussia Dortmund ya Ujerumani hapo jana, City ikiwa haijapoteza mechi hata moja kwenye mechi 4 za ufunguzi katika dimba la klabu bingwa barani Ulaya.

Phil Foden alifunga mara 2 huku Erling Haaland akiunga bao lake la 5 katika mashindano hayo msimu huu, na kumfanya mchezaji wa kwanza katika historia ya klabu bingwa barani Ulaya kufunga katika mechi 5 mfululizo kwa timu 3 tofauti.

Waldemar Anton aliifungia Dortmund bao la kufuta machozi kabla ya Ryan Cherki kuzima matumaini ya klabu hiyo ya Ujerumani kurejea mchezoni dakika za mwisho kwa kuifungia City bao la 4.

Vijana hao wa Pep Guardiola wana pointi 10 katika mechi 4, wakiwa katika nafasi ya 4 nyuma ya viongozi Bayern Munich, Arsenal na Inter Milan walio na pointi 12 kila mmoja.

Inter walirejea kileleni kufuatia ushindi wao wa mabao 2-1 dhidi ya kairat Almaty ya Kazakhstan.

Carlos Augusto aliipa Inter bao la ushindi, baada ya Ofri Arad wa Almaty awali kufuta uongozi wa Inter waliokuwa wamechukua kupitia kwa Lautaro Martinez.

Katika matokeo mengine, Barcelona walitoka nyuma mara 3 na kuondoka na pointi 1 kwenye sare ya mabao 3 dhidi ya Club Brugge, mabao ya Lamine Yamal, Ferran Torres na bao la kujifunga la Christos Tzolis yakiwaondolea aibu miamba hao wa Uhispania.

Hali sawa ilishuhudiwa katika mtanange baina yay a Chelsea na Qarabag, Alejandro Garnacho akifunga bao la kusawazisha kwenye sare ya mabao 2.

Wakati uo huo, bao la kichwa lake Dan Burn liliwahakikishia Newcastle United ushindi wa mabao 2-0 nyumbani dhidi ya Athletic Bilbao, bao jingine likifungwa na Joelinton.

Benfica yake Jose Mourinho ilipoteza mechi yake ya 4 mfululizo kufuatia kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Bayer Leverkusen, huku Ajax wakisalia bila ushindi baada ya mechi 4 kufutia kichapo cha mabao 3 ya Victor Osimhen yaliyoipa Galatasaray ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ajax.

Osimhen anaongoza kwa ufungaji wa magoli msimu huu akiwa amefunga mara 6, mara moja zaidi ya Erling Haaland, Harry Kane na Kyllian Mbappe. 

Imeatayarishwa na Antony Nyongesa

MAN CITY WASHINDA HUKU BARCELONA WAKISHIKWA

STARS KUMENYANA NA SENEGAL MWEZI HUU

MAN CITY WASHINDA HUKU BARCELONA WAKISHIKWA

UFADHILI MDOGO WAONGEZA MADAI YA FIDIA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *