#Sports

KWALE KUANDAA MASHINDANO YA MBIO ZA BAISKELI

Kaunti ya Kwale inajiandaa kuandaa mashindano ya bara la Afrika ya
mbio za baiskeli za barabarani yatakayofanyika kwa siku tatu kuanzia
Novemba 19 hadi 23
Mashindano hayo yanatarajiwa kuvutia waendesha baiskeli nyota
kutoka angalau mataifa 20 ya Afrika pamoja na washiriki wengine
kutoka sehemu mbalimbali duniani, yakilenga kusherehekea vipaji,
nguvu za vijana na umoja kupitia michezo.
Akizungumza wakati wa kikao cha maandalizi katika makao makuu ya
kaunti ya kwale Gavana Fatuma Achani amesema maandalizi
yanaendelea vizuri, huku akisisitiza kuwa usalama na miundombinu
imeimarishwa kuhakikisha mashindano yanafanyika kwa amani na
mafanikio.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *