#Football #Sports

EAGLES WA NIGERIA WAPAA HADI FAINALI

Timu ya taifa ya soka ya Nigeria maarufu kama Super eagles itapapurana kucha na Leopards wa DR Congo kwenye fainali ya kusaka tiketi ya kushiriki mwondoano dhidi ya timu kutoka mabara mengine, kwenye safari ya kuelekea kwenye kipute cha kombe la dunia mwaka ujao.

Mabao 2 ya mshambulizi wa Galatasaray Victor Osimhen katika muda wa ziada yaliwahakikishia ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya Gabon, baada ya mechi hiyo kuishia sare ya goli 1 katika muda wa kawaida jana usiku.

Bao lake Mario Lamina wa Gabon lilifuta bao lake Akor Adams dakika za mwisho, na kulazimisha mechi hiyo kuishia katika muda wa ziada.

Nigeria watarejea katika uwanja wa Stade Prince Heritier Moulay Hassan kumenyana na DR Congo Jumapili waliopata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Indomitable Lions wa Cameroon.

Bao la DR Congo lilifungwa na wing’a wa klabu ya Lille Chancel Mbemba dakika za majeruhi.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *