WAZIRI MKUU AONYA KUWA WAKENYA WALIO NA UJUZI WA MITANDAO YA MAGENDO KUWA TISHIO KWA TAIFA
Waziri Mkuu Musalia Mudavadi ameonya kwamba baadhi ya Wakenya waliookolewa kutoka kwa mitandao ya magendo Kusini-mashariki mwa Asia sasa wanaweza kuwa tishio kwa usalama wa taifa.
Mudavadi aMEsema serikali inazidi kuwa na wasiwasi kwamba baadhi ya waathiriwa, ambao walipata mafunzo ya uhalifu wa mtandaoni wakiwa wamenaswa kutokana na ulaghai wa mtandaoni, wanaweza kutumia ujuzi huo kuanzisha shughuli za ulaghai nchini Kenya.
AMEsema mamia ya wananchi wanaendelea kuteswa na matangazo ya uwongo ya kazi ambayo yanawavutia kufanya kazi za kulazimishwa, ulaghai wa mtandaoni na shughuli zingine haramu katika nchi kama vile Thailand, Vietnam, Kambodia na Myanmar.
Imetayarishwa na Jones Koikai
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































