#Athletics #Sports

FAITH CHEROTICH KUFUNGUA MSIMU WA 2026 KWA MBIO ZA 5000M


Bingwa wa dunia wa mbio za mita 3000 kuruka viunzi, Faith Cherotich, anatarajiwa kufungua msimu wake wa 2026 kwa kushiriki mbio za mita 5000 katika mkutano wa Riadha wa Athletics Kenya utakaofanyika Kapsabet mwezi Machi.

Kocha wake, Bernard Rono, amesema Cherotich yuko katika hali nzuri ya mazoezi, huku programu yake ya maandalizi ikirekebishwa kidogo kufuatia msimu bora wa 2025 uliompa mafanikio makubwa.

Kwa kuwa mbio za mita 3000 kuruka viunzi hazijajumuishwa katika Mashindano ya Dunia ya World Athletics Ultimate ya mwaka 2026 yatakayofanyika Budapest, Cherotich anatarajiwa kuelekeza nguvu zake katika msururu wa Diamond League kama sehemu ya ratiba yake kuu ya mashindano msimu huu.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

FAITH CHEROTICH KUFUNGUA MSIMU WA 2026 KWA MBIO ZA 5000M

KOCHA DE ZERBI AONDOKA MARSEILLE

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *