#Football #Sports

GOR MBIONI KUIMARISHA KIKOSI

Mwenyekiti wa Gor Mahia Ambrose Rachier amethibitisha kwamba wachezaji zaidi wapo njiani kuelekea kwene klabu hiyo, baada ya kumsajili Jackson Dwang kutoka Posta Rangers Jumatano wiki hii.

Kulingana na Rachier, klabu hiyo imemwagiza mkufunzi Charles Akonnor kutambua sehemu zinazohitaji kuimarishwa kikosini na kuchukua hatia mara moja.

Mwenyekiti huyo amepinga taarifa kwamba Dwang amechukua nafasi ya kiungo Austin Odhiambo aliyeondoka, akisema kwamba Dwang ameingia kama sehemu ya kuimarisha safu ya kati.

Odhiambo amekamilisha uhamisho wa kujiunga na klabu ya Nejmeh FC nchini Lebanon.

Gor kwa sasa wanashikilia nafasi ya 2 wakiwa na pointi 26, nyuma ya mahasimu wao wa jadi AFC Leopards wanaoongoza wakiwa na pointi 27 kwenye msimamo wa ligi ambayo inaendelea hii leo.

Kwenye ratiba ya leo, KCB FC watamenyana na Police FC huku Sofapaka wakilenga kusaka namna ya kubaki kwenye ligi mwishoni mwa msimu watakapovaana na Bidco United.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

GOR MBIONI KUIMARISHA KIKOSI

ROBO FAINALI ZA AFCON KUANZA LEO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *