#Football #Sports

MAN U WAPIGWA NA WACHEZAJI 10

Matumaini ya Manchester United kushiriki dimba la klabu bingwa bara Ulaya msimu ujao yamepigwa breki na kichapo cha goli 1-0 na Everton ugani Old Trafford usiku wa kuamkia leo.

Bao la pekee la mchezo lilifungwa na Kiernan Dewsbury-Hall dakika ya 29, baada ya Idrissa Gueye wa Everton kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 13, wakilazimika kulinda uongozi wao wakiwa wachezaji 10.

Gueye alionyeshwa kadi hiyo baada ya kutaka kumzaba kofi mwenzake Michael Keane kutokana na jinsi walivyozuia shambulizi la United.

United waliingia mchezoni wakijua ushindi utawarusha katika nafasi ya 5, ila Everton ambao mara ya mwisho kupata ushindi Old Trafford ulikuwa mwaka wa 1992, walizima matumaini hayo, licha ya mashambulizi ya baadaye ya United yaliyopanguliwa na kipa Jordan Pickford.

Aidha, ushindi huo ulikuwa wa kwanza kwa mkufunzi David Moyes akiwa mgeni uwanjani humo katika mechi za ligi kuu.

Kwa mwenzake wa United Ruben Amorim, atahitaji bidii kuwaondoa vijana wake katika shimo wanaloendelea kujichimbia, kichapo hicho kikihitimisha msururu wa mechi 5 bila kupoteza.

United wamesalia katika nafasi ya 10, pointi 11 nyuma ya viongozi Arsenal.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MAN U WAPIGWA NA WACHEZAJI 10

GOR WALENGA KUDUMISHA UONGOZI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *