#Sports

SERIKALI KUWAZADI MAGWJI WA DEAFLYMPICS

Serikali inatarajiwa kutuza kikosi kilichowakilisha Kenya katika mashindano na Deaflympics jijini Tokyo, Japan na shilingi milioni 36 baada ya kikosi hicho kutia fora katika mashindano hayo na wanamichezo wasio na uwezo wa kusikia.

Akizungumza baada ya kuwakaribisha nchini wanamichezo hao katika uwanja wa JKIA, katibu mkuu katika wizara ya michezo Elijah Mwangi amesema serikali itawatuza kulingana na medali walizovuna kwenye mashindano hayo.

Kenya ilipata jumla ya medali 15, zikiwemo dhahabu 5, fedha 6 na shaba 4.

Kulingana na Mwangi, mshindi wa dhahabu atapokea kitita cha shilingi milioni 3, milioni 2 kwa mshindi wa fedha na milioni 1 kwa mshindi wa shaba, huku mshikilizi wa rekodi ya dunia akikabidhiwa shilingi milioni 5.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

SERIKALI KUWAZADI MAGWJI WA DEAFLYMPICS

SLOT ASISITIZA ATAINUSURU LIVERPOOL

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *