#Local News

MASENETA WATAKA KESI ZA SHERIA YA SUKARI KUHARAKISHWA

Kundi la Maseneta kutoka maeneo yanayolima miwa limewasilisha ombi kwa Jaji Mkuu Martha Koome likitaka mahakama kuharakisha kusikilizwa kwa kesi zinazochelewesha utekelezaji wa Sheria ya Sukari Na. 11 ya mwaka 2024.

Wabunge hao wakiongozwa na Kiongozi wa Wengi katika Seneti Aaron Cheruiyot, pamoja na Maseneta wengine 16 kutoka kaunti za ukanda wa miwa, wanasema mizozo ya kisheria inayoendelea inachelewesha mageuzi yaliyolenga kufufua sekta ya sukari inayokumbwa na changamoto.

Katika ombi lao kwa Jaji Mkuu, Maseneta hao wameonya kuwa ucheleweshaji huo unaendelea kuwaathiri wakulima na wadau wa sekta hiyo waliokuwa wakitarajia mfumo mpya wa kisheria kuleta uthabiti katika tasnia ya sukari.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *