#Local News

IPOA YACHUNGUZA KIFO KITUO CHA POLISI

Mamlaka huru ya kuchunguza mienendo ya polisi IPOA imeanzisha uchunguzi kufuatia kifo cha mshukiwa aliyeripotiwa kujitoa uhai katika kituo cha polisi cha Kisumu central.

Kulingana na taarifa ya polisi, mwili wa mwendazake aliyetambuliwa kama Kelvin Oduor ulipatikana ukiwa unaninginia kwenye dirisha la bafu la kituo hicho cha polisi.

Marehemu alikuwa amekamatwa kwa madai ya wizi na vurugu na kushtakiwa kabla ya mahakama kuamrisha azuiliwe kwa siku 14 kukamilisha uchunguzi.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

IPOA YACHUNGUZA KIFO KITUO CHA POLISI

OGAMBA AWARAI WAHADHIRI KUELEWA HALI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *