#Local News

SARAH WAIRIMU ATAKA KESI YAKE IANZE UPYA

Mahakama kuu inatarajiwa kutoa uamuzi wake kuhusiana na Sarah Wairimu, mshukiwa mkuu wa mauaji ya mumewe raia wa Uholanzi Tob Cohen, anayetaka iagize kesi ya mauaji dhidi yake inayoendelea katika mahakama kuu za Kibra ifutiliwe mbali na kuanza kusikilizwa upya.

Katika ombi lake, Wairimu anahoji kuwa vikao vya kesi hiyo vimekumbwa na dosari mbali na ukiukaji wa katiba na taratibu za kisheria, akitaka uamuzi na amri zote ambazo zimetolewa hadi sasa kwenye kesi hiyo kuondolewa, mbali na kusikilizwa na jaji tofauti na wala si Diana Kavedza.

Ameiomba mahakama kulifanya ombi lake kuwa la dharura.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *