MAHANGAIKO YA WAGONJWA WA KANSA
Wagonjwa wa saratani nchini sasa wanalazimika kununua dawa nje ya hospitali licha ya kusajiliwa na bima ya afya SHA kutokana na uhaba wa dawa kwenye hospitali mbali mbali za umma.
Baadhi ya wagonjwa hao katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta na AIC Kijabe, wamesema uhaba huo pia umeshuhudiwa kwa vifaa vingine vya matibabu.
Sasa wameitaka bima ya SHA kuongeza mgao wa matibabu yao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 

















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































