WATAHINIWA WA KJSEA KUREKEBISHA SHULE
Wanafunzi wanaojiunga na gredi ya 10 katika shule za sekondari ya juu wamepewa fursa ya kufanya marekebisho ya shule walizowekwa na serikali kuanzia kesho, baada ya kuripotiwa dosari ikiwemo baadhi ya wanafunzi kuwekwa kwenye shule za jinsia zisizofaa.
Katibu katika idara ya elimu ya msingi Julius Bitok, amesema zoezi hilo la siku 7 litafanyika katika shule ambazo wanafunzi hao walifanyia tathmini ya gredi ya 9, tangazo lake likijiri baada ya malalamishi ya wazazi.
Dosari nyingine ni wanafunzi kuwekwa kwenye shule za kutwa zilizo mbali na nyumbani kwao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 

















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































