#Sports

KOCHA WA AFC LEOPARDS, FRED AMBANI, AMEMSIFU MSHAMBULIAJI VICTOR OMUNE

Kocha wa AFC Leopards, Fred Ambani, amemsifu mshambuliaji
wa Harambee Stars, Victor Omune, kwa mchango wake muhimu
uliowasaidia Ingwe kuibuka na ushindi wa 2–1 dhidi ya Shabana
FC katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Gusii.
Ushindi huo umeendeleza rekodi ya kutopoteza mechi kwa
Leopards kwenye Ligi Kuu ya SportPesa 2025, huku ukiongeza
presha kwa Shabana ambao sasa hawajashinda katika mechi nne
mfululizo.
Shabana walitangulia kupata bao kupitia Austin Odongo, kabla
Omune kusawazisha baada ya kupokea pasi murua kutoka kwa
Julius Masaba.
Bao la kujifunga lililosababishwa na kona ya James Kinyanjui
liliipa Leopards pointi tatu muhimu katika pambano hilo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

KOCHA WA AFC LEOPARDS, FRED AMBANI, AMEMSIFU MSHAMBULIAJI VICTOR OMUNE

VINICIUS AOMBA RADHI KWA MASHABIKI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *