KENYA TAYARI KUWAKILISHA U-21 TAEKWONDO
Timu ya Kenya iko tayari kung’ara nyumbani wakati Mashindano ya
Dunia ya Taekwondo ya Wachezaji Chini ya Miaka 21 yanapoanza hii
leo katika Ukumbi wa Kasarani Indoor Arena.
Kikosi cha wachezaji 16 kimekuwa kikijifua katika Kenya Academy of
Sports, na kiko tayari kutoa maonyesho ya kuvutia mbele ya
mashabiki wa nyumbani.
Mashindano haya ya kwanza kabisa yamevutia mataifa 77 na zaidi ya
wanariadha 450, yakiongeza hamasa kubwa kimataifa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































