RUTO AWATAKA MAGAVANA KUHARAKISHA MAGEUZI MUHIMU
Rais William Ruto amezitaka serikali za kaunti kuongeza kasi katika kutekeleza mageuzi muhimu, akionya kwamba kuchelewesha hatua hizo kunaendelea kudumaza mafanikio kamili ya ugatuzi licha ya hatua kubwa zilizopigwa kitaifa.
Akizungumza baada ya kuongoza Mkutano wa 12 wa Mashauriano kati ya Serikali ya Taifa na za Kaunti katika Ikulu ya Nairobi, Ruto amesema ushirikiano kati ya ngazi hizo mbili za serikali umeleta maendeleo ya maana, lakini bado kuna kazi kubwa mbele kuhakikisha wananchi wanahisi athari za huduma zilizogatuliwa moja kwa moja katika maisha yao ya kila siku.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































