KCSE 2025: IDADI YA A PLAIN YAONGEZEKA
Jumla ya watahiniwa 1,932 wa mtihani wa KCSE mwaka jana walipata alama ya A plain kwenye mtihani huo, ikiwa ni ongezeko la gredi hiyo ikilinganishwa na watahiniwa 1,693 waliopata A plain mwaka 2024.
Haya ni kulingana na matokeo ya mtihani wa KCSE 2025 ambayo yametangazwa na Waziri wa elimu Julius Ogamba, akisema idadi ya watahiniwa waliopata alama ya C+ na zaidi iliongezeka kutoka 246,000 mwaka 2024 hadi 270,000 kwenye mtihani wa mwaka jana.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































