POLISI WAHIMIZA MADEREVA KUMAKINIKA BARABARANI
Madereva wamehimizwa kuchukua tahadhari wanapokaribia maeneo ya Gilgil na Kikopey kwenye barabara kuu ya Nairobi- Nakuru kufuatia visa vya ajali ambapo watu 7 wameaga dunia huku wengine 11 wakijeruhiwa kwenye ajali iliyohusisha magari kadhaa.
Kamanda wa polisi eneo la Gilgil Winson Mwakio, amethibitisha ajali hiyo na kuwataka madereva kuwa makini ili kudhibiti visa vya ajali.
Walioshuhudia wamelalamikia ongezeko la ajali eneo hilo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































