TWAHIR MUHIDDIN, AMEPONGEZA MWENENDO WA GOR MAHIA,
Aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Harambee Stars, Twahir
Muhiddin, amepongeza mwenendo wa Gor Mahia, akisema viongozi
hao wa Ligi Kuu ya Soka Kenya (KPL) wanaonekana kuwa katika hali
bora ya kutwaa tena ubingwa walioupoteza kwa Kenya Police FC
msimu uliopita.
Gor Mahia, maarufu kama K’Ogalo, kwa sasa wana alama 16,
wakiongoza ligi kwa tofauti ya pointi moja mbele ya Kakamega
Homeboyz, baada ya kushinda mechi tano kati ya saba.
Twahir alisifu ushawishi wa kocha mpya kutoka Ghana, Charles
Akonnor, akisema ujio wake umeleta ari mpya, nidhamu na morali
kubwa ndani ya kikosi cha Gor Mahia — mambo ambayo, kwa mujibu
wake, yanaifanya timu hiyo ionekane “kutozuilika” msimu huu.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































