PETER WANYAMA AKUBALI MATOKEO LSK
Wakili Peter Wanyama amekubali matokeo ya uchaguzi wa chama cha wanasheria nchini LSK wa hapo jana ambapo alimaliza wa pili nyuma ya mshindi Charles Kanjama, ila akalalamikia alichokitaja kuwa kutojitolea kwa mawakili kushiriki uchaguzi huo.
Wanyama ambaye alitangaza kuwania kiti hicho Septemba mwaka jana, amesisitiza kuwa uongozi unahiaji unyenyekevu katika kushinda na kushindwa.
Amesema licha ya mawakili wanaohudumu kuwa 18,000 kati ya 26,000 walio wanachama wa LSK, ni 8,600 pekee waliojitokeza kupiga kura.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































