KAHATA AWEKA MATUMAINI KWA KCB
Kiungo mshambuliaji wa zamani wa Gor Mahia, Francis Kahata, ameonyesha matumaini kuwa bao lake la kwanza litakuwa mwanzo wa mafanikio mema kwa klabu yake mpya huku nusu ya pili ya ligi ikianza.
Kiungo huyo mkongwe alipachika bao wakati KCB iliposhinda Posta katika ushindi muhimu uliopatikana kwenye Uwanja wa Kasarani
Bao hilo lilikuwa la kwanza la ligi kwa kahata huku akisema mafanikio hayo ni mwanzo wa mwelekeo mpya wanapolenga kupanda juu kwenye msimamo wa ligi na kupata matokeo zaidi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































