#Local News

DHAHABU YA IKOLOMANI ITAWAFAIDI WAKAZI, BUNGE LAAHIDI

Bunge la kaunti ya Kakamega limewahakikishia wakazi wa eneo la Ikolomani kwamba litalinda maslahi yao wakati wa uchimbaji wa madini ya dhahabu ambao umeratibiwa kuanza hivi karibuni na mwekezaji wa kibinafsi.

Spika wa bunge hilo James Namatsi, amekiri kuwa bunge hilo limepokea malalamishi ya wakazi walio na hofu ya kudhulimiwa wakati wa zoezi hilo ambalo limezingirwa na utata.

Ameahidi vikao na usimamizi wa kampuni itakayochimba dhahabu hiyo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

DHAHABU YA IKOLOMANI ITAWAFAIDI WAKAZI, BUNGE LAAHIDI

PETER WANYAMA AKUBALI MATOKEO LSK

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *