UPASUAJI WA MIILI YA MAFURIKO KUFANYWA
Zoezi la upasuaji wa miili ya watu waliofariki kutokana na mafuriko wiki jana jijini Nairobi imeratibiwa hii leo katika makafani ya City, baada ya miili hiyo kutambuliwa huku idadi ya waliofariki kote nchini ikifikia watu 44.
Familia za walioangamia zimekuwa zikifika katika makafani hayo tangu Jumamosi kwa lengo la kuwasaka na kuwatambua jamaa zao waliosombwa na maji ya mafuriko Ijumaa usiku.
Serikali ya kaunti ya Nairobi imefutilia mbali bili zote za hospitali kwa waathiriwa wa mafuriko hayo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































