POLICE BULLETS WAREJEA KILELENI BILA MECHI
Kenya Police Bullets wamerejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake ya FKF-WPL baada ya kupewa ushindi wa mezani kufuatia wapinzani wao waliopangwa kukutana nao, KISPED Queens, kushindwa kufika kwa mechi hiyo.
Ushindi huo wa mezani yaani walkover, uliotolewa Jumatano, umeipeleka Bullets kileleni wakiwa na pointi 22 baada ya mechi 10, na hivyo kufungua pengo dogo la pointi moja dhidi ya Vihiga Queens wanaoshikilia nafasi ya pili wakiwa na pointi 21.
Matukio hayo yanaendelea kuleta ushindani mkali katika kusaka taji la ligi hiyo, Bullets wakipambana kwa karibu na Vihiga Queens na Ulinzi Starlets
Vihiga Queens ni miongoni mwa timu zinazopigiwa upato kunyakua taji hilo, huku Ulinzi Starlets na Trinity Starlets wakifuata kwa karibu katika nafasi ya 3 na 4 wakiwa na pointi 20.
Kayole Starlets ambao pia wamonysha kuimarika pakubwa, wanafunga nafasi ya 5 bora wakiwa na pointi 16 baada ya mechi 10.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































