MATUKIO YA KCSE 2025
Ukiukaji wa kanuni za zinazoongoza mitihani ya kitaifa ni miongoni mwa visa viliyoripotiwa kwenye siku ya kwanza ya mtihani wa kidato cha 4 KCSE hapo jana, mwalimu mkuu mmoja katika kaunti ya Narok akisimamishwa kazi kwa muda ili kupisha uchunguzi dhidi yake.
Kulingana na mkuu wa elimu katika kaunti hiyo Apollo Apuka, mwalimu huyo alipatikana akivunja mwongozo wa baraza la mitihani KNEC, ingawa hakuweka wazi ukiukaji maalum.
Wakati uo huo, shule moja kwenye kaunti ya Kajiado inachunguzwa kwa madai ya wizi wa mtihani.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































