#Local News

IEBC KUSAMBAZA VIFAA VYA UCHAGUZI

Maandalizi ya chaguzi ndogo za Alhamisi wiki ijayo yameingia hatua za mwisho, tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC ikitarajiwa kuanza usambazaji wa vifaa vya kupiga kura kuelekea maeneo hayo hii leo.

Kupitia taarifa, IEBC imesema miongoni mwa vifaa hivyo ni karatasi na masunduku ya kupigia kura, helikopta zikitumiwa kusafirisha vifaa hivyo katika maeneo yaliyo mbali kutoka Nairobi na yanayokabiliwa na changamoto za kiusalama kama vile Banisa.

Shehena ya mwisho ya vifaa hivyo kutoka Ugiriki imepokelewa na makamishna wakiongozwa na Hassan Noor Hassan na Ann Nderitu.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *