WATOTO 164 WALIFARIKI HOSPITALINI KIAMBU, DUALE
Watoto waliokuwa wakitaka kuzaliwa pamoja na mama zao ndio walioathirika pakubwa na mgomo wa madaktari katika kaunti ya Kiambu, zaidi ya Watoto 160 na akina mama zaidi ya 10 wakiaga dunia wakati wa uzazi katika kipindi cha mgomo huo.
Akizungumzia athari za mgomo huo mbele ya bunge la kitaifa, Waziri wa afya Aden Duale amethibitisha ripoti ya muungano wa madaktari KMPDU kwamba idadai kubwa ya Watoto wachanga walifariki wakati wa kuzaliwa licha ya serikali ya kaunti ya Kiambu kukana hapo awali.
Aidha, Wakazi walilazimika kusaka huduma nje ya kaunti hiyo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































