RUTO AAHIDI “NEW SINGAPORE”, UPINZANI WAMKEJELI
Rais William Ruto amesisitiza kwamba angali na mpango wa kuimarisha Kenya kiuchumi na kuifanya iwe miongoni mwa mataifa yaliyostawi ulimwenguni, akiwataka wakenya kuwapuuza walio na shauku kuhusu mpango huo.
Akizungumza katika eneo la Maralal kaunti ya Samburu, Rais Ruto ametetea hoja hiyo, akisema ana mpango maalum wa kufanikisha ndoto hiyo.
Wakati uo huo, viongozi wa upinzani wamemkosoa Ruto kwa madai ya kulemaza sekta muhimu kama vile elimu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































