WAFANYABIASHARA ZAIDI YA 1,000 GITHURAI WAPOTEZA VIBANDA
Zaidi ya wafanyabiashara 1,000 katika Soko la Githurai wanakadiria hasara kubwa baada ya vibanda vyao kubomolewa alfajiri ya Alhamisi kupisha ujenzi wa kituo cha mabasi.
Operesheni hiyo ilitekelezwa na Mamlaka ya Kitaifa ya Barabara Kuu Kenya (KENHA), siku moja tu baada ya wafanyabiashara hao kuandamana kupinga mpango wa ubomoaji.
Ingawa walikuwa wamepewa notisi ya kuondoka, wamelalamikia serikali kwa kutowapatia maeneo mbadala ya kufanyia biashara kabla ya ubomoaji kufanyika.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































