SESKO AWEKA HAI MATUMAINI YA UNITED UEFA MSIMU UJAO
Benjamin Sesko alifunga bao la pekee la mchezo na kuwapa Manchester United ushindi muhimu na pointi 3 ugenini dhidi ya Everton jana usiku, na kuwaweka vijana hao wa Michael Carrick katika nafasi ya 4.
Sesko alifunga bao jingine muhimu siku 13 zilizopita na kulazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya West Ham, na mara tena alifanya hivyo katika dakika ya 71 hapo jana baada ya kuingia kama nguvu mpya.
Kiungo huyo wa Slovenia amefunga mabao 8 tangu kuwasili kwake, na cha kushangaza ni kwamba ni mabao 2 pekee kati ya hayo yalifungwa chini ya Reuben Amorim, na 3 chini ya kocha wa muda Darren Fletherna 3 chini ya Carrick.
Everton walitishia pointi za United mara kadhaa, ila United wakaokolewa na Senne Lamens mchumani.
Kwa sasa United wana pointi 48 katika nafasi ya 4, pointi 3 mbele ya Chelsea na Liverpool katika nafasi ya 5 na 6 mtawalia, na 3 nyuma ya Aston Villa Villa katika nafasi ya 3.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 

















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































